Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na Serikali ya Nepal washirikiana kuhifadhi Lumbini alikozaliwa Budha

hekalu,nguzo,dimbwi na mabaki. Picha@UNESCO/Junko Okahashi

UNESCO na Serikali ya Nepal washirikiana kuhifadhi Lumbini alikozaliwa Budha

03hapanapalenepalunescobudha.mp3

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni, UNESCO likishirikiana na serikali ya Nepal leo wametia saini mkataba wa miaka mitatu ili kukamilisha awamu ya pili ya mradi wa kuimarisha na kulinda Lumbini ambapo ni mahali pa kuzaliwa kwa Bwana Budha na Urithi wa Dunia. Mradi huo unafadhiliwa na serikali ya Japan.

Mradi huo utatekelezwa na Ofisi ya UNESCO ilioko Kathmandu ikishirikiana na idara ya elimu ya mabaki ya kale, pamoja na shirika la ustawi na maendeleo ya Lumbini litakalosaidia Nepal kuhifadhi sehemu hiyo ambayo imeorodheshwa kama sehemu ya Urithi wa Dunia tokea mwa wa 1997.

Hii ikiwa pamoja na sehemu ya akiolojia ya Tulaurakot- mabaki ya utawala wa mfalme Shakya na Ramamgramana, pamoja na mabaki au kumbukumbu ya Bwana Budha, ni maeneo mawili yanayoaminika kuhusiana na maisha ya Bwana huyo, ambayo yametengwa na kuorodheshwa kama Urithi wa Dunia.