Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC kujadili maendeleo endelevu baada ya 2015

UN Photo/Paulo Filgueiras
Rais wa ECOSOC kwa mwaka wa 2014, Martin Sajdik. Picha@

ECOSOC kujadili maendeleo endelevu baada ya 2015

Tukielekea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, linaendesha wiki hii mkutano wa viongozi wa kisaisa kuhusu maendeleo endelevu, unaoshirikisha nchi wanachama, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akiuhutubia mkutano huo, rais wa ECOSOC, Martin Sajdik, amewakumbusha washiriki kuhusu umuhimu wa mkutano huo akisema umefika wakati mwafaka:

“ Hivi sasa, tunasonga mbele katika juhudi zetu za mwisho ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Mkutano huo utasaidia kuonyesha utashi wetu wa kutokomeza umaskini na kutimiza maendeleo endelevu kwenye kipindi cha mwisho cha msafara wetu kuelekea 2015. Lakini hasa itatusaidia kutathmini utekelezaji wa MDGs na kuandaa Zaidi malengo ya maendeleo endelevu”.

Akisikitishwa kwamba baadhi ya nchi wanachama hawajaukubalia umuhimu wa mkutano huo, amewaomba washiriki kujitahidi kufanikisha mjadala huo ili kuonyesha manufaa yake, akisema:

“ Nimejaribu kuandaa mkutano huo kama sehemu mwafaka ya kufuatilia malengo na ahadi za baada ya 2015. Leo najisikia kama baba alipata mtoto. Nataka pia kuwashukuru wakunga wengi ambao wamesaidia katika uzalishaji huo. Sasa naamini kwamba pamoja tutalea mkutano huo kutoka utotoni hadi uzima”