Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres kwa Waislamu: Ramadhan Karimu na endeleeni kuwasaidia Wakimbizi

Guterres kwa Waislamu: Ramadhan Karimu na endeleeni kuwasaidia Wakimbizi

Wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan ukiwa ndio umeanza, Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres, ametuma salamu zake kwa Waislamu wote na kuwatakia mfungo mwema, huku akisema kuwa mwaka huu mwezi wa Ramadhan umekuja wakati ulimwengu unaposhuhudia ongezeko la watu waliolazimika kuhama makwao kwa viwango ambavyo havijashuhudiwa katika miongo mingi.

Bwana Guterres amesema kutoka Mali, Sudan Kusini, Syria hadi Afghanistan, watu zaidi ya milioni 50 sasa wamelazimika kuhama makwao, wengi wao wakiwa wanatoka au wanapewa hifadhi katika nchi za Kiislamu,

“Na nyingi ya nchi hizo zimeonyesha ukarimu mkubwa, katika moyo wa mshikamano na ulinzi wa wanyonge, ambao unatokana na utamaduni wa uislamu, kama ilivyoandikwa katika Koran takatifu na mafundisho ya Mtume Mohamed, Amani iwe naye. Na nina imani kuwa usaidizi huu utaendelea. Nawatakia tena na familia zenu mwezi mtukufu wa Baraka. Ramadhan karimu.”