Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa wasiwasi na hali mashariki mwa Ukraine

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Ban atiwa wasiwasi na hali mashariki mwa Ukraine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezwa kuendelea kutiwa wasiwasi na hali mashariki mwa Ukraine, ingawa pia amekaribisha hatua zinazochukuliwa kurejesha utulivu, zikiwemo mashauriano yanayojumuisha pande zote na kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa siku tatu zaidi.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imesema kuwa Bwana Ban anatarajia pande zote kutimiza ahadi zao, na kutoa wito kwa wahusika wote kufanya juhudi za kukomesha machafuko kupitia harakati za kisiasa.

Katibu Mkuu pia amekaribisha kuachiwa huru waangalizi wanne wa OSCE mnamo tarehe 26 Juni, na kutoa wito wanne wengine ambao bado wanazuiliwa waachiwe huru.