Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahofia wakimbizi wa DRC kurudi nyumbani kwa safari binafsi

Wakimbizi kutoka DRC kwenye kituo cha Nyakabande, Uganda. Picha@UNHCR/L.Beck(UN News Centre)

UNHCR yahofia wakimbizi wa DRC kurudi nyumbani kwa safari binafsi

Nchini Uganda, Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja  Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR, ameguswa na taarifa za wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuendelea kutoroka makambi na kurudi nyumbani ki-vyao.

 Tarifa kamili, na John Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchiniUganda.

 (TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakimbizi wa DRC wasiopungua 1,000 wamerudi nyumbani kivyao kutoka makambi mbali mbali ya mpakani.

 Mnamo mwezi Februari, wakimbizi 108 walipoteza uhai wao baada ya boti walimokuwa wakisafiria kurudi nyumbani kivyao kuzama katika Ziwa Albert.

 Sakura Atsumi, Naibu Mwakilishi wa UNHCR humo nchini ameguswa na taarifa kwamba licha ya hali hiyo mbaya kutokea wanaendelea kujirudisha nyumbani wakitumia njia hatarishi.

 (Sauti Sakura Atsumi)

 “Hata baada ya ajali, baadhi ya wakimbizi wameedelea kurudi nyumbani kivyao. Kwa sababu wanarudi  kivyao, wanatumia njia hatarishi, kwa mfano boti zisizo salama kwenye Ziwa na magari yasiyo salama”

 (Sauti Sakura Atsumi)

Amewataka wawe na subira akisema UNHCR na serikali zaUgandana DRC wanapanga kuwarudisha nyumbani kwa njia salama.

 ”Tunawaomba wawe na subira ndiyo mpango wa kuwasaidia kurudi nyumbani kwa njia salalma uanze, warudi salama”

 Kuna takriban wakimbizi 180,000 wa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hapa Uganda.