Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka nchi za Afrika kulinda haki za binadamu

Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha: Eskender Debebe/Equatorial Guinea.

Ban azitaka nchi za Afrika kulinda haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo ametoa wito kwa nchi za bara la Afrika kuheshimu na kulinda Haki za Binadamu, wakati akiuhutubia mkutano wa viongozi wa Afrika mjini Malabo, nchini Equatorial Guinea. Taarifa kamili na Joshua Mmali

 Taarifa ya Joshua

Katika hotuba yake, Ban ameusifu msimamo uliochukuliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, AU, katika kukabiliana na mashambulizi na mateso yanayowalenga walinda haki za binadamu, na kukaribisha uamuzi wa kuutangaza mwaka wa 2016 kuwa Mwaka wa Afrika wa Haki za Binadamu, hususan haki za wanawake.

Katibu Mkuu amesema ni lazima ziongezwe kasi juhudi za kuwalinda wanawake dhidi ya ukatili, na kulinda hakiyaoya kushiriki katika masuala yote yanayoihusu jamii kwa njia ya usawa na wanaume.

Ban ameongeza kuwa ili kuliwezesha bara la Afrika, itabidi kuwezesha umma, kuwezesha usawa wa jinsia na kuheshimu haki za binadamu.

Aidha, amesema kuwa kuibadilisha na kuiendeleza Afrika kutahitaji nishati endelevu kwa wote, kubadilisha mifumo ya uzalishaji wa kilimo kupitia kurekebisha sera na teknolojia.

Amesifu pia azimio la Umoja wa Afrika la kutokomeza njaa na utapiamlo ifikapo mwaka 2025.