Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan achieni huru wafungwa kwa kisiasa: Mtaalamu

Mashood Adebayo Baderin. (Picha@Jean-Marc Ferré)

Sudan achieni huru wafungwa kwa kisiasa: Mtaalamu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu nchini Sudan Mashood Adebayo Baderin amesema kuwa serikali inawajibu wa kuweka mazingira rafiki yatayowezesha watu wote kushiriki siasa bila kubinywa na hali yoyote.

Pia ameitolea mwito Serikali ya Sudan kuwaachia huru wafungwa wote wa kiasiasa ili kufungua ukurasa mpya wa amani na maridhiano kwa watu wote.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake ya siku tano nchini humo, Adebayo Baderin amesema kuwa serilali inapaswa kuanzisha duru la maridhiano kwa kuwaachia wafungwa hao wa kisiasa.

Hivi karibuni Serikali iliwatia mbaroni wanasiasa kadhaa akiwamo kiongozi wa chama cha Umma Sadiq Al-Mahdi kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya uchochezi.