Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Iraq ni tete, ISIL yaweka sharia kwa maeneo yaliyotekwa

Hali nchini Iraq ni tete, ISIL yaweka sharia kwa maeneo yaliyotekwa

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, Nickolay Mladenov, amesema hali ya kiusalama na kisiasa nchini Iraq ni tete tangu kunyakuliwa kwa mji wa Mosul na wanamgambo wa ISIL, ambao sasa wameyateka maeneo mengi ya Iraq yenye Wasunni wengi. Taarifa kamili na Joshua Mmali

 (Taarifa ya Joshua)

Bwana Mladenov, ambaye amewahutubia waandishi wa habari mjini New York kwa njia ya video kutoka Baghdad, amesema miji mikubwa, ikiwemo Mosul, Tikrit, na Faluja na kuanza kuweka sheria ya Uislamu wenye msimamo mkali, na kufanya mauaji ya kinyama

“Tumeona ripoti kadhaa za mauaji ya halaiki ya wanajeshi wa serikali wa Kishia, na kuwang’oa raia wa Kishia. Mauaji haya pia yamekuwa yakiwalenga wafungwa, hususan katika mkoa wa Diyala”

Bwana Mladenov amesema wanaendelea kutoa msaada bila kupendelea upande wowote, pamoja na kuchunguza hali ya Haki za Binadamu, ambazo zimekiukwa kwa kiasi kikubwa na pande zote katika mzozo huo. Amesema kujua idadi kamili ya wahanga wa kiraia kunakabiliwa na matatizo ya kiusalama na usafiri