Ujumbe wa UM Cote d’Ivoire waongezewa mwaka mmoja zaidi

25 Juni 2014

Baraza la Usalama limepitisha azimio leo mjini New York la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d’Ivoire, UNOCI, kwa kipindi cha mwaka moja.

Rais wa Baraza hilo Vitaly Churkin akitangaza matoeko ya kura baada ya kupigiwa kura akisema kura zote 15 zimeunga mkono hatua hiyo na azimio ni namba 2162 la mwaka 2014.

Azimio pamoja na kuongeza muda limepongeza ujumbe huo na kazi zilizofanywa chini ya uongozi wa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Bi Aichatou Mindaoudou kwa kuchangia kurejesha hali ya usalama nchini humo. Jitihada zinazohitajika hivi sasa, kwa mujibu wa azimio hilo, ni pamoja na kubadilisha mfumo wa uraia na umiliki wa ardhi na kutayarisha uchaguzi unaotakiwa kufanyika Oktoba, mwakani.

UNOCI imepewa mamlaka ya kusaidia serikali ya Cote d’Ivoire katika maandalizi hayo, baraza la usalama likiwaomba viongozi wa kisaisa kuachana na maneno ya chuki na kikabila. Halikadhalika walinda amani wa UNOCI wanatakiwa kupunguzwa, baraza la usalama likitarajia kufunga UNOCI baada ya uchaguzi wa mwaka 2015, hali ya usalama ikiruhusu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter