Tanzania yapazia sauti Mkataba wa Bamako kuhusu uteketezaji wa kemikali za sumu:

25 Juni 2014

Mwakilishi wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi, Dkt. Batilda Buriani amesema ni matumaini  yake kuwa mkutano wa Baraza la mazingira duniani unaoendelea nchini Kenya utaibuka na mkakati madhubuti wa kusimamia utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa Bamako kuhusu udhibiti na uteketezaji wa taka za sumu barani Afrika.

Dkt. Batilda ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa kando kwa mkutano wa UNEA.

(Sauti ya Dkt. Batilda)

Mwakilishi huyo pia akagusia pia suala la kuongeza bajeti ya UNEP ili iweze kutekeleza jukumu lake.

(Sauti ya Dkt. Batilda)

Mkataba wa Bamako ulipitishwa mwaka 1991 na ulianza kutekelezwa mwaka 1998

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud