Skip to main content

Stadi za ujasiriamali zawezesha wanawake kuvuna matunda ya amani Somalia:ILO

Picha@ILO

Stadi za ujasiriamali zawezesha wanawake kuvuna matunda ya amani Somalia:ILO

Shirika la kazi duniani, ILO limeanzisha mradi wa kuwapatia stadi za ujasiriamali wanawake huko Somaliland kama njia mojawapo ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Mradi huo unaofadhiliwa pia na Umoja wa Ulaya ulianza mwaka jana ambapo miongoni mwa wanufaika ni Zaynab Ahmed ambaye sasa anaendesha biashara ya matunda na mboga za majani.

Zaynab amesema kabla ya kupata stadi hizo biashara ilikuwa ya hasara kwani hakuweza kutunza mahesabu, kufungasha bidhaa zake na hta kushirikiana na wajasiriamali wenzake. Hata hivyo  hivi sasa yeye na wanawake wengine 150 wamejiunga kwenye kikundi chini ya mradi wa kuendeleza usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake Somalia na stadi wanazoapatiwa zimewaimarisha.

Mshauri Mkuu wa kiufundi wa ILO nchini Somalia Paul Crook amesema wananchi wameweza kuweka mazingira ya amani sasa wanachohitaji ni maendeleo ya kiuchumi ili waweze kuvuna matunda ya amani. Chini ya mradi huo wanawake wanapatiwa stadi za msingi kuhusu usimamizi wa biashara ili waweze kuendesha biashara zao kwa faida na wakati huo huo ziwe endelevu kwa maisha yao na mazingira.