Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yataka kuongeza operesheni zake Mali: yahitaji ufadhili

Huduma ya lishe bora ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto. (Picha@WFP)

WFP yataka kuongeza operesheni zake Mali: yahitaji ufadhili

Tukielekea Mali, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP linapanga kuongeza msaada wake kwa raia wa Mali ili kufikia watu zaidi ya Laki Nane  kati ya mwezi huu na Oktoba, iwapo chakula kitakosekana kipindi hicho.

WFP inasema, zaidi ya watu milioni 1.5 wameathirika na ukosefu wa chakula, shida ikiwa si kukosa chakula pekee, bali pia watu kukosa pesa za kununua vyakula.

Ingawa kuzorota kwa hali ya usalama kaskazini mwa nchi hiyo kumesababisha mashirika mengine kupunguza idadi ya wafanyakazi wao, WFP imeendelea kusambaza vyakula kwenye maeneo hayo.

WFP inatoa wito ili kufadhili operesheni zake nchini Mali, likikiri kukosa zaidi ya asilimia 65 ya mahitaji yake ya pesa.