Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ilikuwa ngumu lakini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa:Kaag

UN Photo/Devra Berkowitz
Sigrid Kaag @

Kazi ilikuwa ngumu lakini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa:Kaag

Mratibu maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali OPCW Sigrid Kaag amesema jukumu walilokamilisha la kuondoa silaha za kemikali za sumu Syria lilikuwa ni zito lakini ushirikiano wa kimataifa umewezesha kufanikisha.

Bi. Kaag amesema hayo katika mahojiano maalum na Reem Abaza wa Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya OPCW kutangaza hatua hiyo iliyoelezwa kuwa ni  ya kipekee.

(Sauti ya Kaag)

Hili lilikuwa jukumu zito kwani lilijumuisha wadau wa aina tofauti kukiwa na operesheni ndani ya nchi, kutoa vifaa, kuthibitisha na kulinganisha kutoka maeneo mbali mbali ambayo wakati mwingine ilikuwa vigumu kuyafikia. Hali mbaya ya usalama na pia kazi yenyewe ya kusafirisha kupeleka kwenye bandari. Na kuwasili kwenye meli za Norway na Denmark, na hatimaye kuhamishia kwenye meli ya Marekani ambayo ilikuwa inateketeza kwa njia maalum. Sasa ukiweka yote hayo na unatekeleza kwenye nchi wakati wa vita, unaona changamoto tulizopata wakati wa kupanga na kutekeleza. Lakini tumeweza kufanikisha kwa kufikia asilimia 100 ya kuondoa silaha za kemikali.

Bi. Kaag amesema jukumu walilokuwa wamekabidhiwa lilikuwa ni la kipekee na jamii ya kimataifa na mamlaka zaSyriazinapaswa kupongezwa na kwa ujumla limekuwa la mafanikio.

Amesema mwelekeo sasa ni tathmini inayoendelea ya ripoti ya Syriakuhusu kutokomeza mpango wao wa silaha za kemikali na pia wanasubiri uamuzi wa baraza tendaji la OPCW juu ya uteketezaji wa tani hizo za silaha zilizoondolewa Syria.