Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi kutoka DRC ashinda tuzo kwenye kambi ya Kyangwali, Uganda

Mshindi wa tuzo ya mwanamke mkimbizi, Zawadi Gahima akionyesha tuzo yake baada ya kukabidhiwa. (Picha:John kibego@Radiowashirika Spice FM)

Mkimbizi kutoka DRC ashinda tuzo kwenye kambi ya Kyangwali, Uganda

Maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani huko Uganda hususan kambi ya wakimbizi ya Kyangwali yalifana kwa kushuhudia mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Mwanamke huyo amefanya mengi ikiwemo kuanzisha vikundi vya kuwezesha wanawake wakimbizi kuwa na maisha endelevu na zaidi ya yote wanaume kusaidia kupigania haki za wanawake. Je mwanamke huyo ni nani? Basi ungana na John Kibego wa Radio washirika Spice FM kutoka Uganda katika makala hii.