Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili kutoka ndani na jamii ya kimataifa ni msingi wa amani endelevu

UN Photo/Martine Perret
Ujenzi wa amani Timor Leste @

Ufadhili kutoka ndani na jamii ya kimataifa ni msingi wa amani endelevu

Tukielekea makao makuu ya Umoja waMataifa,New York, leo Tume ya Ujenzi wa Amani iiladhiimisha siku ya Ujenzi wa Amani kwa kuendesha mjadala maalum kuhusu ufadhili wan chi zinazojijenga baada ya vita. Taarifa Zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Maudhui hayo yalichaguliwa kwa ajili ya mkutano huu wa kwanza wa tume ya ujenzi wa Amani, mwenyekiti wake Antonio de Aguiar Patriota akisema, ukosefu wa pesa ndiyo moja ya changamoto zinazokumba nchi zilizo kwenye kipindi cha mpito baada ya mizozo, ukiweza kusababisha vita kuanza upya.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Jan Eliasson amesema utawala bora na ukusanyaji wa mapato ndiyo msingi kwa ujenzi wa Amani.

“ Nchi zilizokumbwa na mizozo zinahitaji zaidi pesa na usaidizi wa kisiasa na uongozi.  Mapigano yakiisha, bado vidonda vya vita vinaumiza.  Msaada wa kimataifa ni lazima, lakini hausaidii kujenga nchi na jamii kwa muda mrefu na endelevu. Njia bora ya kusaidia nchi zilizo kwenye kipindi cha mpito baada ya mizozo ni kuzisaidia kukusanya mapato yao na kujijengea uwezo wao wenyewe". 

Ametolea mfano wa Burundi na Rwanda ambazo zilifanikiwa kujijenga upya baada ya vita kwa kuboresha mifumo yao ya kukusanya mapato na ushuru, na kuimarisha utawala bora.