Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Mashariki ya Kati

Mkuu wa masuala ya siasa ndani ya UM, Jeffrey Feltman (Picha@Maktaba UM)

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao kilichojikita katika kujadili suala la amani katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.

Kikao hicho kimehutubiwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman, ambaye amesema kuwa matatizo mengi ya Ukanda wa Gaza bado yanahitaji masuluhu ya kimfumo ambayo hayajapatikana.

Bwana Feltman amezungumza pia kuhusu Lebanon, akitoa wito kwa viongozi wake wafanye uchaguzi wa rais mpya bila kuchelewa. Suala la mzozo wa Syria pia limemulikwa, Bwana Feltman akirejelea ujumbe wa Katibu Mkuu wiki iliyopita.

 

SAUTI YA FELTMAN