Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera kuhusu misitu zihusishe zaidi wananchi ili ziwe endelevu: FAO

UN Photo/Logan Abassi
upandaji wa miti Haiti @

Sera kuhusu misitu zihusishe zaidi wananchi ili ziwe endelevu: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeanza kikao chake kinachomulika masuala ya misitu huku ripoti yake mpya ikitoa wito kwa nchi kuweka sera zitazosaidia zaidi kuendeleza sekta ya misitu ili kuimarisha maeneo kama ya chakula, afya na nishati. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

 Kikao hicho ambacho kinaundwa na wajumbe wa kamati ya misitu pia kimeshudia Mtoto wa mfalme wa Ubelgiji Laurent akichaguliwa kuwa balozi maalumu wa FAO katika maeneo ya misitu na mazingira.

China ya wadhifa huo, jukumu lake kubwa litakuwa ni kuelimisha umma na kuleta mwamko juu  ya mambo yanayohusu misitu na mazingira.

Pia kikao hicho kimepokea ripoti maalumu iliyozinduliwa ikielezea hali ya misitu duniani ikitaka mabadiliko ya kisera ili kuhusisha zaidi wananchi katika usimamizi wa misitu. Ewald Rametsteiner ni afisa mwandamizi wa Misitu FAO.

(Sauti ya Ewald)

Imezoelekea kuwa misitu ni mali ya umma na serikali ndio inadhibiti. Wananchi wao ni kuchukua rasilimali kama kuni na kadhalika na hawahusiki sana na menejimenti. Kwa hiyo mabadiliko ya sera za usimamizi ni muhimu na yanafanyika polepole lakini ni vyema iboreshwe na kasi iongezwe ili kuwapatia wananchi manufaa zaidi kutokana na bidhaa na  huduma za misitu.”

Kikao hicho kilichoanza leo kinatazamiwa kumalizika Juni 27.