Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa lazinduliwa Nairobi

Ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kenya. Picha@UNEP

Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa lazinduliwa Nairobi

Mamia ya mawaziri wa Mazingira, watunga sera, wanasayansi, wawakilishi wa umma na wafanyabiashara leo wamekusanyika mjini Nairobi, Kenya kwa mkutano wa uzinduzi wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA), ambalo litakuwa na jukumu la kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira katika ajenda ya ushirikiano wa kimataifa, na kutoa msukumo mpya wa kukabiliana na matatizo ya dunia. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

 Uzinduzi wa Baraza la Mazingira unachukuliwa kama upeo wa juhudi za kulifanya suala la mazingira kuwa lenye umuhimu mkubwa kwa ulimwengu mzima, kwani sasa kwa mara ya kwanza litachukuliwa kama linalolingana na masuala mengine kama amani, usalama, fedha, afya na biashara.

Baraza hilo ambalo linafanya kikao chake cha kwanza kwenye makao makuu ya Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, linalenga kumulika masuala muhimu kama vile biashara haramu ya viumbe wa porini, ubora wa hewa na uchafuzi wa mazingira, utawala wa sheria katika mazingira, ufadhili wa uwekezaji unaojali mazigira, pamoja na malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Waiganjo njoroge ni Afisa mawasiliano wa UNEP mjiniNairobi.

(Sauti ya Waiganjo)