Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rekodi mpya yawekwa wakati Siku ya Wakimbizi Duniani ikiadhimishwa

Wakimbizi wa CAR walioko Cameroon. (Picha@Unifeed)

Rekodi mpya yawekwa wakati Siku ya Wakimbizi Duniani ikiadhimishwa

Wiki hii, Umoja wa Mataifa umeadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, mnamo Ijumaa tarehe 20 Juni, huku Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akisema kwamba, kote duniani, mizozo imewalazimu watu kukimbia makwao kwa idadi iliyovunja rekodi.

Ban amesema kuwa wakati huo huo, mizozo mingine ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu bado haijatatuliwa, ikimaanisha kuwa watu wachache tu ndio wameweza kurudi nyumbani kwao.

Miongoni mwa wachache waliobahatika kurudi nyumbani, ni wakimbizi waBurundi, ambayo ni moja ya nchi ambazo miaka ya nyuma zilishuhudia wimbi kubwa la raia wake wakikimbia machafuko na kuwa wakimbizi katika nchi jirani  hususanTanzaniana DRCongo. Sasa taifahilolimeanza kustawi kiusalama na hivyo kuvutia sehemu kubwa ya wakimbizi wake kurudi makwao. Hata hivyo changamoto kubwa ni kuwakwamua tena kimaisha  warejeaji hao, ambao wengi wao wamepotezamalizao huku wengine wakikosa ardhi.

Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA ametembelea kituo cha muda  cha Mutambara  kusini mwa nchi kunako pokelewa wakimbizi hao na kutuandalia makala hii.

(Sauti: Mutambara.mp3)

PRISCILLA: Tukitoka Bujumbura, tunakwenda hadiGeneva, ambako,kamasehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR, limetoa ripoti inayoonyesha kuwa idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kwa sababu za kiusalama, imeongezeka kote duniani na kuzidi watu milioni 50 kwa mara ya kwanza tangu vita vikuu vya pili.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, asilimia 86 ya wakimbizi hao wanaishi katika nchi zinazoendelea. Barani Afrika, nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini naSomalia, ndizo zilizoathiriwa na tatizo la wakimbizi wengisanakatika siku za hivi karibuni. Hapa, Joshua Mmali anatupsha zaidi, na kutuletea sauti za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchiniKenyanaUganda