Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya wakimbizi nchni Iraq bado hayajafikishwa.

@UNHCR/ C. Robinson

Mahitaji ya wakimbizi nchni Iraq bado hayajafikishwa.

Mashirika ya kimataifa ya msaada ya kibinadamu yamesema, mahitaji ya watu waliolazimika kukimbia makwao nchini Iraq hayajahudumiwa ipasavyo.

Miongoni mwa mashirika hayo ni lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ambalo linasema idadi ya wakimbizi nchini humo imefikia Milioni moja, likisema wengi wanahifadhiwa na familia ilhali wengine wameanza kutafuta hifadhi kwenye kambi zinazojengwa hivi sasa.

Msemaji wa UNHCR, Adrian Edwards, amesema wana wasiwasi kuhusu wakimbizi 100,000 wa Syria waliosaka hifadhi magharibi mwa Iraq kutokana na mapigano yaliyotokea karibu na kambi ya Al Qaem.

Tayari UNHCR imesambaza mahema, magodoro, tenki za maji, vifaa vya kupika na kujisafi, wakati shirika la mpango wa chakula duniani likisema linajipanga kuongeza misaada yao kwa Irraq kufikisha wakimbizi wapya.

Halikadhalika, Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu nchini Iraq, Jacqueline Badcock, ameziomba pande zote za mzozo kutozuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa wanaoihitaji, akiongeza kuwa, watu waliokimbia Mosul wiki iliyopita bado wanahitaji chakula na maji, wengi wakiwa wamekosa malazi.