Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za uwajibikaji bora wa kampuni kwa jamii zinatenga wanawake:Ripoti

Ukumbi wa baraza la haki za binadamu, Geneva Uswisi@UN Multimedia

Juhudi za uwajibikaji bora wa kampuni kwa jamii zinatenga wanawake:Ripoti

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linachofuatilia ubaguzi dhidi ya wanawake kisheria na kivitendo limesema mwelekeo ulioibuka wa uwajibikaji wa kampuni kwa jamii unaathiri wanawake.

Ripoti ya kundi hilo kwa Baraza la Haki za binadamu iliyowasilishwa huko Geneva leo imesema kuanzishwa kwa maeneo ya kutengeneza bidhaa za kuuza nje ya nchi, mazingira mabovu ya kazi, sheria ya kulipa fidia, maeneo ya ardhi kwa mmiliki pekee ambao mara nyingi ni wanaume ni moja ya njia za uvunjaji wa haki za kibinadamu za wanawake, amesema Frances Raday ambaye ni Mkuu wa kikundi hilo.

Halikadhalika ametaja ongezeko la tofauti ya vipato kati ya wanaume na wanawake kunakotokana na sera za uchumi na kampuni akisema kuwa yamekuwa na madhara makubwa kwa wanawake ambao wako nafasi ya chini.

Bi Raday amesema serikali zina mamlaka kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu kuzuia ubaguzi unaofanywa na kampuni zilizo ndani ya eneo lao.

Ametoa wito kwa serikali kuhakikisha misingi ya uwajibikaji wa kampuni kwa umma unazingatia maslahi tofauti ya wanawke na mahitajiyaona wakati huo huo serikali hizo zitambue na zichukue hatua kuzuia shughuli za kampuni zenye madhara kwa wanawake.