Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakumbuka familia za wakimbizi zilizotawanyika Kenya

Kambi ya wakimbizi ya Dadaab, Kenya. Picha: UNHCR/B.Bannon

UNHCR yakumbuka familia za wakimbizi zilizotawanyika Kenya

Nchini Kenya, maadhimisho ya siku ya wakimbizi yalifanyika katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kaskazini mwa nchi hiyo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudhumia Wakimbizi UNHCR nchini Kenya limekiri kuwapa hifadhi Zaidi ya wakimbizi 500,000 kutoka nchi 15 tofauti katika kambi zake, Kenya ikiwa nchi inayoongoza Afrika kwa kupokea wakimbizi.

Sherehe iliyofanyika ndani ya kambi ya Dabaab ilikusanya vikundi vya wasanii wa asili mbalimbali, nyota wa Hip Hop Kenya OtcoPizzo, pamoja na viongozi na mabalozi kadhaa.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu yakiwa ni familia moja kugawanyika kwa vita inakithiri, Ofisi ya UNHCR Kenya imechukua fursa ya siku hiyo kukumbusha watu kuhushu hali ya wakimbizi waliopo Kenya, ambao wamekamatwa na polisi kurejeshwa kambini mapema mwezi wa Aprili mwaka huu.

Kitendo hicho kilifanyika kufuatia visa vya ugaidi vilivyotokea Kenya, na serikali kuchukua hatua ya kutaka wakimbizi wote waliokuwa mjini, kupelekwa katika kambi za Dabaab au Kakuma. Operesheni hiyo imewakamata maelfu ya wakimbizi, na karibu watoto 300, kuanzia umri wa miezi miwili, wakiripotiwa kutawanywa kutoka kwa wazazi wao.