Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Wapalestina isisahaulike

@UNRWA

Hali ya Wapalestina isisahaulike

Wakati wa Maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Pierre Krahenbuhl, ametaka jamiii ya kimataifa iwakumbuke wakimbizi wa Palestina waliopo Syria, ili wasisahaulike. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

Pierre Krahenbuhl  amesema, nusu ya wakimbizi hawa 550,000 waliotafuta hifadhi nchini Syria wameathirika na mzozo unaonedelea nchini humo, nusu ya kambi zao 12 zikiwa zimegeuka sehemu za mapigano.

Halikadhalika, wafungwa wa Palestina walioanza mgomo wa kususia chakula ili kushutumu hali yao ya kufungwa nchini Israel bila mashtaka wala kesi, wako kwenye hali mbaya zaidi, kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu. Msemaji wa ofisi hii, Ravina Shamdasani, ameiomba serikali ya Israel iheshimu haki zao na ama iwaruhusu au iwafungulie mashtaka, lakini, isiwazuie kuendelea na mgomo  wa kususia chakula:

“Kamishna Mkuu amemwandikia Mwakilishi  wa kudumu wa Israel  katika umoja wa mataifa nchini Geneva akielezea wasiwasi wake kwamba sheria mpya ikipitishwa, basi itaruhusu kulishwa kwa nguvu na kuwatibu wafungwa walio susia chakula bila hiari yao, na hii itakuwa ukiukwaji wa maadili za kimataifa.