Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Syria ni sababu kuu ya idadi ya wakimbizi iliyovunja rekodi: Ban

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Mzozo wa Syria ni sababu kuu ya idadi ya wakimbizi iliyovunja rekodi: Ban

Wakati huo huo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon ametoa ujumbe wake wa siku hii ya Wakimbizi Duniani, akisema kote duniani, mizozo imewalazimu watu kukimbia makwao kwa idadi iliyovunja rekodi.

Ban amesema kuibuka tena mapigano katika nchi za Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini pia iliwang’oa watu kutoka makwao, akisema kuwa asilimia 86 ya wakimbizi wote duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea.

Katika ujumbe huo uliochapishwa kwenye Intaneti, Ban amesema mwaka uliopita pekee, zaidi ya watu milioni kumi walilazimika kuhama makwao, familia moja ikikimbia kila dakika kumi na tano, akiongeza kuwa mzozo wa Syria ni mojawapo ya sababu kuu ya ongezeko hili la idadi ya wakimbizi.

Hii leo mjini New York, Bwana Ban ameihutubia jamii ya watu wa Asia mjini New York kuhusu mzozo huo wa Syria.