Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaombwa kusaidia huduma za afya Kurdistan, Iraq

Picha: WHO/S. Al-Dahwi — Iraq.

WHO yaombwa kusaidia huduma za afya Kurdistan, Iraq

Wizara ya Afya ya Mkoa wa Kurdistan nchini Iraq imeripoti kuwepo uhaba wa dawa na kutoa ombi kwa Shirika la Afya Duniani WHO kuipa usaidizi ili iweze kupata dawa na huduma zinazohitajika kwa dharura.

Mkoa huo hupokea dawa na vifaa vya kutoa chanjo kutoka serikali kuu Baghdad, lakini sasa haiwezi tena kupokea vifaa hivyo na dawa tangu machafuko yalipoanza, kwa sababu za kiusalama na barabara kutopitika.

Tangu machafuko yalipoanza, WHO imekuwa ikitoa usaidizi wa vifaa vya matibabu kwa halmashauri za Dohuk na Erbil, mkoani Kurdistan, na sasa inajaribu kutafuta njia endelevu zaidi za kuhakikisha kuna dawa za matibabu na chanjo, kwani sasa inatarajiwa kuwa mgogoro huo wa Iraq utaendelea.