Wajumbe wa Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya raia Iraq

19 Juni 2014

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng na yule anayehusika na wajibu wa kulinda raia, Jennifer Welsh, wameelezea kusikitishwa mno na hali inayoendelea nchini Iraq.

Wajumbe hao wamelaani vikali mashambulizi yanayowalenga raia ambao hawahusiki na uhasama kamwe, wakisema kuwa mashambulizi kama hayo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Wameongeza kuwa ukiukwaji huo unaweza kuorodheshwa kuwa uhalifu wa kivita.

Wamesema pia kuwa kuzorota kwa usalama kumeongezwa na makundi ya kigaidi kama lile la ISIL na mengineyo nchini humo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter