Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mizozo mitatu mipya imewafanya mamilioni kuwa wakimbizi:WFP

Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Ertharin Cousin. Picha: WFP(UN News Centre)

Mizozo mitatu mipya imewafanya mamilioni kuwa wakimbizi:WFP

Siku moja kabla ya Siku ya Wakimbizi Duniani, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa dunia tayari inakabiliwa na mizozo mitatu mipya yenye madhara makubwa, na ambayo imewageuza mamilioni ya watoto wa shule, wakulima na wafanya biashara kuwa wakimbizi.Taarifa kamili na Amina Hassan…

(Taarifa ya Amina Hassan)

Siku moja baada ya kuizuru kambi ya Wakimbizi ya Zaatari nchini Jordan, Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Ertharin Cousin amesema kuwa machafuko mapya nchini Iraq yamewalazimu watu nusu milioni kutoroka makwao na kuwa sehemu ya takriban watu milioni 45.2 ambao wamelazimika kuhama makwao kote duniani.

Mnamo mwaka 2013, WFP iliwasaidia wakimbizi milioni 4.2 na wakimbizi wa ndani milioni 8.9 kote duniani, ikisaidiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR.

Wengi wa wakimbizi hao na watu waliolazimika kuhama makwao walitokana na mizozo ya Syria, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bi Cousin amesema wakati ghasia Iraq zikiibuka, ulimwengu unafaa kukumbuka kuwa mizozo kama ya hiyo haiharibu tu maisha ya wale wanaokimbia, bali pia inachangia umaskini kwa jamii zinazowapa hifadhi.