Mbuga ya Selous yaorodheshwa kwenye urithi wa asili ulio hatarini duniani: UNESCO

18 Juni 2014

Kamati ya Urithi wa Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO, ikikutana leo mjini Doha, Qatar, imeingiza mbuga ya Hifadhi ya Wanyama ya Selous, kusini mashariki mwa Tanzania katika orodha ya Urithi wa Dunia ulio Hatarini, kwa sababu ya ujangili wa kupindukia.

Mbuga ya Selous ambayo ina eneo la kilomita 50,000 mraba, ni moja ya mbuga kubwa Zaidi barani Afrika, ambayo inajulikana kwa kupatikana kwa tembo, vifaru weusi, duma, twiga, viboko, mamba, na wanyama pori wengine. Pia mbuga hiyo ina aina nyingi tofauti ya viumbe wa pori, vikiwemu miombo, msitu, sehemu za nyasi, kinamasi… ikisemekana kuwa mbuga hiyo ni maabara ya mabadiliko ya kibayolojia na kiekolojia.

Lakini, ujangili unaoendelea umesababisha kupungua idadi ya wanyama pori, hasa kwa upande wa tembo na vifaru, ambao idadi yao imepungua kwa asilimia 90 tangu 1982, wakati mbuga hiyo iliorodeshwa katika Urithi wa Dunia.

Mkutano wa Urithi wa Dunia ukiendelea mpaka tarehe 15, Juni, wanachama wametoa wito kwa nchi ambazo ama zinasafirisha au zinapokea pembe za tembo kushirikiana na Tanzania ili kutokomeza uhalifu huo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter