Umoja wa Mataifa wazindua muongo wa maendeleo endelevu kwa wote Asia na Pasifiki

18 Juni 2014

Umoja wa Mataifa umezindua leo mwongo wa maendeleo endelevu kwa wote katika eneo la Asia na Pasifiki, katika hafla ambayo imefanyika mjini Manila, Ufilipino. Kwa kutambua haja ya kufikisha nishati endelevu kwa wote, Umoja wa Mataifa ulizindua mwongo wa nishati endelevu kwa wote (SE4ALL), 2014-2024, ukizingatia umuhimu wa nishati katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Wakati huo huo, Kamisheni ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Asia na Pasifikia, ESCAP, ikishirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, na Benki ya Maendeleo ya Asia, ADB, yamezindua ofisi ya kikanda ya kuratibu masuala ya nishati kwa ngazi ya kitaifa.

Inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni 628 katika eneo la Asia na Pasifiki, ambao ni takriban nusu ya idadi nzima ya watu wenye umaskini wa nishati duniani, hawana huduma za umeme, na zaidi ya watu bilioni 1.8 wanatumia mbinu za kijadi kama vile kuni.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter