Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa takwimu mpya za maambukizi ya virusi vya Ebola Afrika Magharibi

WHO yatoa takwimu mpya za maambukizi ya virusi vya Ebola Afrika Magharibi

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani, imesema kuwa kati ya tarehe 14 – 17 Juni mwaka huu, kumekuwa na visa vipya vya ugonjwa wa Ebola nchini Guinea na watu 7 wanasadikika kufariki dunia na kuongeza jumla ya idadi ya watu waliofariki kufikia 398 nchini humo. Zaidi ya watu 1,258 wanaendelea kufuatiliwa.

Nchini Sierra Leone, takwimu zinaonyesha maambukizi mapya ya watu 31 ambayo yamesababisha vifo vya watu wanne kati ya tarehe 15 na 17 Juni, na hivyo kufikisha jumla ya watu 97 kufariki dunia.

Liberia nayo imekuwa na hali hiyo hiyo na ripoti zinasema kuwa kati ya tarehe 11hadi 17 Juni, nchi hiyo iimpoteza watu 24 na kuna visa 9 vipya ambazo zimeripotiwa na jumla ya watu 108 ziko kwa orodha ya kufuatiliwa nchini humo.

Shirika la Afya duniani na wadau wake limesema kuwa kuna visa vipya ambavyo vimeripotiwa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone na hivyo basi, limezisihi Serkiali za nchi hizo kuweka mikakati ya kuzuia uwenezaji wa ugonjwa huo kupitia kwa zahanati na vituo vya afya.

Ujumbe wa Shirika hilo unafanya lolote uwezalo kusitisha usambazaji wa ugonjwa huo katika ukanda huo wa Afrika Magharibi kwa kushirkiana na wizara za afya, na limetuma kundi la madaktari kuangazia na kufuatilia kwa makini ili kudhibiti athari za ugonjwa wa virusi vya Ebola.

Mkutano mkubwa unaoshirikisha nchi hizo tatu utafanyika tarehe 23 Juni mwaka huu.