Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kirusi cha Corona chapiga hodi Iran:WHO

Nembo ya shirika la afya duniani, WHO. @WHO

Kirusi cha Corona chapiga hodi Iran:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limepokea taarifa juu ya kugundulika kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya virusi vya Corona nchini Iran.

Ripoti zinasema kuwa uchunguzi wa kimaabara umebaini kuwepo watu wawili wameambukizwa virusi hivyo ambavyo kuathiri mifumo ya upumiaji na maeneo mengine ya mwili.

Watu hao ni mtu na dada yake wanaishi katika jimbo la Kerman na inaarifiwa kwamba wao hawajawahi kusafiri nje ya nchi lakini walikutana na mtu ambaye alisafiri kwenda Saudi Arabia kwa Hija.

Hakuna taarifa zaidi zilitolewa mbali ya WHO kutaka wananchi kuwa waangalifu hasa wakati virusi hivyo vikisambaa katika eneo hilo.