Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia watoroka makwao kwa hofu ya mapigano Iraq-IOM

Mamia ya wananchi huko Mosul wakihama makwao, Picha@IOM IRAQ

Mamia watoroka makwao kwa hofu ya mapigano Iraq-IOM

Shirika la Kimataifa linalohusika na wahamiani IOM nchini Iraq limesema kuwa limepokea taarifa kuwa zaidi ya raia 500,000 waliokuwa wakiishi katika eneo linalojiongoza la Ninewa huko Mosul wameyakimbia makazi yao.

Shirika hilo limefichua kuwa sababu kubwa iliyowafanya raia hao kukimbia maskani zao ni kutokana na wasiwasi wa kuongezeka mapigano yanayoendeshw ana kundi moja la waasi lenye shabaha ya kulitwaa eneo hilo.

Hivi karibuni kulizuka mapigano makali katika eneo hilo yaliyohusisha vikosi vya serikali na kundi hilo la waasi na kusabisha mamia ya watu kujeruhiwa.

Kumewekwa hali ya tahadhari katika eneo hilo kama jaribio la kudhibiti hali yoyote korofi toka kwa makundi ya waaasi.