Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yataka mchakato wa uchaguzi uzidi kuimarishwa

UN Photo/Paulo Filgueiras
Jan Kubis@

UNAMA yataka mchakato wa uchaguzi uzidi kuimarishwa

Wakati duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchiniAfghanistaninatarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi huu wa Juni na maandalizi yakiendelea, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA umewahimiza wahusika wote watimize majukumu zao kwa thati kwa ajili ya raia waAfghanistan.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afghanistan Ján Kubiš amesema kuwa duru hiyo ni tukio la kipekee linalothibithisha kuwa demokrasia inaonyesha nuru nzuri nchini humo.

Bwana Kubis ambaye pia ni mkuu wa UNAMA ameelezea kuwa  duru ya kwanza ya tarehe 5 Aprili, ilionyesha maendeleo makubwa ilikinganishwa na uchaguzi uliopita lakini kumekukwa na matatizo madogo na udhoofu wa hapa na pale na hivyo ni vyema kuhakikisha duru  ya pili inaridhisha raia wa nchi hiyo.

Kwa kuwa uchaguzi unagusa maeneo mawili muhimu; kisiasa na ile ya kiteknolojia, bwana Kubis amewasihi wahusika wawe waangalifu ili kutimiza malengo ya wapiga kura kwa kuweka wazi na mawasiliano ya kutoa matokeo  ya uchaguzi na pia kusuluhisha mambo yote kwa njia bora ili kujenga imani ya watu wa nchi hiyo na pande zote zinazohusika.

Amesema kuwa teknolojia pekee siyo suluhu ya uchaguzi huu, bali wagombea pia wako na jukumu muhimu ya kukubali matokeo kwa kuhamasisha wafuasi wao wasijiingize kwa matendo za ulaghai.

Washika dau wote walikutana  tarehe 9 Juni, na wakatoa hakikisho kwa Bwana Kubis kuwa watatekeleza majukumu zao ipasavyo.