Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhai wa mama na mtoto kwenye kambi za wakimbizi Sudan Kusini mashakani

(Picha@Unifeed)
Mhudumu wa afya akimpima mtoto wa punde baada ya kujifungua. (Picha@Unifeed)

Uhai wa mama na mtoto kwenye kambi za wakimbizi Sudan Kusini mashakani

Takwimu zaonyesha kuwa Mmoja kati ya wanawake 7 nchini Sudan Kusini hufariki dunia akiwa mjamzito au wakati anapokwenda kujifungua. Hivyo kuifanya nchi hiyo  changa kuwa moja ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya vifo vya wajawazito duniani. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linasema nchini Sudan Kusini mtoto wa kike yuko hatarini mara tatu zaidi kufariki dunia wakati wa kujifungua kuliko kuingia darasa la Nane. Je hali ikoje? Basi ungana na John Ronoh kwenye makala hii.