Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yathibitisha mashtaka dhidi ya Bosco Ntaganda

Bosco Ntaganda: Picha ya ICC

ICC yathibitisha mashtaka dhidi ya Bosco Ntaganda

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Jopo la majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai, ICC, leo limethibitisha mashtaka yote 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu dhidi ya Bosco Ntaganda, yakihusisha mauaji na jaribio la mauaji, kuwashambulia raia, majengo yasiyostahili kushambuliwa, uporaji, ubakaji, utumwa wa kingono, kuwaingiza watoto chini ya umri wa miaka 15 katika vita, utesaji na kuwalazimu watu kuhama makwao.

Kwa mantiki hiyo basi, Bwana Ntaganda atawasilishwa kwa koti ya kuendessha mashtaka dhidi yake.

Ntaganda alijisalimisha na kuwasilishwa kwa ICC mnamo Machi 22 2013, na kesi ya kuthibitisha mashtaka dhidi yake ilifanyika mnamo Februari 14, 2014. Ushahidi wa takriban kurasa 69,000 uliwasilishwa kwa jopo la majaji katathminiwa.

Kulingana na ushahidi huo, jopo hilo liliridhika kuwa kulikuwa na mashambulizi ya kupangwa katika jimbo la Ituri, DRC, dhidi ya raia ambao hawakuwa wa kabila la Hema, kama wa makabila ya Lendu, Bira na Nande, kati ya tarehe 6 Agosti 2002 na 27 Mei 2003.