Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya huduma za binadamu yahofia hali ya wakimbizi wa ndani Yemen

Wakimbizi wa Yemen@OCHA

Mashirika ya huduma za binadamu yahofia hali ya wakimbizi wa ndani Yemen

Mashirika ya kutoa Huduma  za binadamu nchiniYemenyamelalamikia hali ya kuzuka kwa vita baina ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo waliojihami mwishoni mwa Mei na mwanzo wa Juni mwaka huu.Vita hiyo imesababishisha watu zaidi ya 20,000 katika jimbo la Amran nchini humo kuhama makaaziyao.

Jambo la kuridhisha kwa sasa ni kwamba makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa  mjini Amran tarehe 4 Juni  yameokana kuhifadhiwa na pande zote mbili, ijapokuwa kuna shida ya kufikisha misaada kwa waathiriwa zaidi ya 40,000 waliotimuliwa makwao na mzozo tangu mwaka wa 2011.

Hadi sasa, barabara kuu itokayo Sana’a mji mkuu waYemenikielekea sehemu iliyokumbwa na vita bado imefungwa. Hata hivyo bado kuna usaidizi wa kibinadamu unaoendelea katika mji wa Amran lakini hakuna kinachoendelea nje ya jiji hilo, na hivyo kusabababisha upungufu wa maji, chakula na huduma za afya  kwa wakaazi wa eneo hilo.

Imeripotiwa kuwa majeruhi  zaidi ya 200 wanapata matibabu kwenye hospitali kuu ya Amran, ambayo haina uwezo ya kuhudumia wagojwa wengi na hivi sasa kumekuwa na upungufu wa madawa ya upazuaji na yale ya kufisha mwili ganzi kwa ajili ya upasuaji.

Hivi sasa, wahudumu wa kibinadamu wametoa msaada kwa hospitali tatu katika sehemu hiyo  na kuna mpango wa kufungua hospitali ya kuhamahama.