Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa jamii za asili wapaza sauti juu ya haki zao, wawekea matumaini mkutano wa Septemba

UN Photo/Rick Bajornas)
Watu wa jamii za asili wakiwa mjini New York, Marekani.( Picha

Watu wa jamii za asili wapaza sauti juu ya haki zao, wawekea matumaini mkutano wa Septemba

Mwezi Mei mwaka huu kikao cha kudumu kuhusu watu wa asili kilifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Mei kikikutanisha aidi ya wawakilishi 1,500 wa watu wa jamii za asili. Washiriki walitoa Asia, Ulaya, Afrika, Amerika na hata Australia na kubwa lililoangaziwa ni hatua zilizochukuliwa kulinda haki za kisiasa, kiuchumi na kijamii za kundi hilo adhimu duniani. Je ni kwa mapana  yapi mjadala ulifanyika? Nini kilikubaliwa? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii