Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo unaweza kuitumbukiza Sudan Kusini katika baa la njaa: WFP

Mzozo unaweza kuitumbukiza Sudan Kusini katika baa la njaa: WFP

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limeelezea wasiwasi yake kwamba mzozo wa Sudan Kusini unaielekeza nchi hiyo kwenye baa la njaa.  WFP imesema mapigano Sudan Kusini yamesababisha ukosefu wa uhakika wa chakula katika maeneo ambayo yametengwa na mzozo huo.

WFP imesema baa la njaa bado linaweza kuepukika, lakini ni muhimu sana mapigano yakomeshwe na kukabiliana na vikwazo vingine vinavyozuia ufikishaji wa misaada ya kuokoa maisha kwa walengwa.

Kufikia sasa, WFP na wadau wake wamefikisha misaada ya kuokoa maisha kwa zaidi ya watu milioni 1.1 walioathiriwa na mzozo katika zaidi ya maeneo 125 Sudan Kusini, na wanajitahidi kukabiliana na pingamizi nyingi sugu ili kuwafikia watu wengi zaidi kila siku. WFP inawasaidia watu wengine laki tatu na nusu ambao wamekimbilia nchi jirani kutoka Sudan Kusini.