Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sayansi ya Nyuklia yawasaidia wakulima Zanzibar kuongeza uzalishaji

Khatib katika kituo cha Kizimbani @IAEA - L. Potterton

Sayansi ya Nyuklia yawasaidia wakulima Zanzibar kuongeza uzalishaji

Wakulima kisiwani Zanzibar wanakuza aina ya mpunga ulibuniwa kwa kutumia teknolojia ya nyuklia. Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, lilitumia mbinu ya miyonzi ya nyuklia kutengeneza aina hiyo mpya ya mpunga iitwayo, SUPA BC.

Mbinu hiyo ambayo imekuwa ikitumika tangu miaka ya 1920, hutumia miyonzi hiyo kubadilisha mimea ili kuongeza uzalishaji na kuifanya ihimili magonjwa na mazingira magumu kama vile ukame.

Khatib Juma Khatib ni Mratibu wa Programu ya Utafiti katika Mpunga kwenye taasisi ya utafiti ya Kizimbani, Zanzibar.

KHATIB

Mpunga aina ya SUPA BC umekuwa ukipandwa tangu mwaka 2011, na tayari umeonyesha matumaini makubwa kwa kuongeza viwango vya uzalishaji.