Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamasha kuhusu mustakhbali bora na endelevu kufanyika kwenye Umoja wa Mataifa

Tamasha la kuweka jukwaa la maendeleo endelevu

Tamasha kuhusu mustakhbali bora na endelevu kufanyika kwenye Umoja wa Mataifa

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Wasanii mashuhuri wa kimataifa wanatazamiwa kuchukuwa jukwaa kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, katika tamasha la muziki wenye ujumbe wa matumaini ya mustakhbali bora zaidi mwaka 2015 na baada ya hapo.

Tamasha hilo la kimataifa linaloandaliwa na Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe, linatarajiwa kutumia nguvu za muziki, ushairi na video, ili kumulika nafasi ya kihistoria itakayojitokeza mwaka 2015, wakati viongozi wa dunia watakapofanya ahadi za kuiweka sayari dunia kwenye mkondo wa kufikia ufanisi zaidi na endelevu, kwa kutangaza malengo la maendeleo endelevu.

 Tamasha hilo litawaleta jukwaani wasanii kadhaa kutoka visiwa vya Karibea, ikiwemo bendi ya muziki wa zouk ya Kassav’ na wasanii wa soca, David Rudder, Machel Montano na Tizzy. Bendi ya Lalon kutoka Bangladesh, inayochanganya muziki wa kitamaduni wa Kibengali na rock pia itatumbuiza. Mwingine anayetarajiwa jukwaani ni Emmanuel Jal, alieyekuwa zamani mtoto vitani Sudan Kusini na ambaye sasa ni msanii wa Hip Hop na mwanaharakati.