“Umuganda” inaleta pamoja jamii:Rwanda

Jeanne d'Arc Byaje, Naibu Mwakilishi katika Ujumbe wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa. @
Wiki hii, Ujumbe wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa uliandaa tukio maalum ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka ishirini ya mauaji ya kimbari, mwaka 1994, Rwanda. Lengo la mkutano, licha ya kukumbuka wahanga na manusura wa uhalifu huo, lilikuwa pia ni kuonyesha jinsi gani Rwanda imeweza kuungana tena, kutunza mazingira na kujenga miundumbinu mipya kupitia mfumo wa zamani wa kazi za kijamii kwa pamoja uitwao umuganda. Je nini kiilifanyika? Basi ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii!