Bado kuna haja na udharura wa kuondoa kemikali za sumu Syria: Kaag

4 Juni 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

Mratibu maalum wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Kupinga Matumizi ya Silaha za Kemikali nchini Syria, Sigrid Kaag, amewasilisha ripoti yake ya kila mwezi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa azimio namba 2118, ambalo lilihitaji kuhakiki na kutokomeza mpango wa silaha za kemikali za taifa la Syria.

Baada ya kulihutubia Baraza la Usalama, Bi Kaag amekutana na waandishi wa habari na kutoa maelezo kuhusu ripoti hiyo, na jinsi harakati za kuondoa na kuteketeza silaha hizo zinavyoendelea, na kwamba sasa asilimia 92.8 ya silaha na kemikali za sumu zimeondolewa

SAUTI YA KAAG

“Tumeashiriwa na mamlaka za Syria kuwa mara tu mazingira ya usalama yatakavyoruhusu, uondoaji silaha kwenye kituo cha pili utaanza. Imebainika pia kuwa hii inatarajiwa kuwa hivi karibuni. Lakini pia nimekuwa nikiwasiliana na mamlaka za Syria Damascus, na tumezungumza pia na baadhi ya mataifa yenye ushawishi kwa pande zinazozozana Syria, ambazo pia zipo kwenye eneo hilo. Kwa hiyo tunatoa wito kwa nchi zote wanachama kutumia ushawishi wao kuhakikisha uondoaji mara moja wa kemikali zote zilizosalia.”

Bi Kaag amesema haja, udharura na shinikizo la kuondoa asilimia 7.2 ya kemikali zilizosalia bado ni muhimu, na kwamba atarejea Damscus katika siku chache zijazo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter