Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkwamo huko Syria ni zaidi ya kuvusha misaada mpakani:Amos

UN Photo/Eskinder Debebe)
Mkuu wa OCHA Valerie Amos.(Picha@

Mkwamo huko Syria ni zaidi ya kuvusha misaada mpakani:Amos

Ugumu wa usambazaji wa misaada ya kibinadamu hukoSyriani zaidi ya uvushaji misaada mpakani, amesema Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kibinadamu, OCHA, Valerie Amos alipozungumza na waandishi wa habari mjiniNew York siku ya Jumatano.

Amos amesema mkwamo kwenye mipaka ni moja tu ya mambo yanayozorotesha ufikishaji misaada kwa mamia ya maelfu ya wahitaji nchini Syria wakati huu ambapo mzozo umeingia mwaka wa nne na kiwango cha ghasia kinazidi kuongezeka.

(Sauti ya Amos)

“Tunapaswa kushughulikia masuala yanayowezesha operesheni zetu ili tuweze kusafiri bila vikwaz na kwa usalama. Hili ni suala la serikali na pia vikundi vilivyojihami vinavyohusika na mapigano. Siwezi kuelezea ugumu wa operesheni tunaopata kwenye kazi yetu. Unaweza kuafikiana na kikundi unachodhani kinadhibiti eneo fulani au vikundi vyote lakini bado unakutana na baadhi ya watu wanaokueleza kuwa hilo haliwezi kufanyika. Tunafikiri tunaweza kufikia watu kati ya Bilioni Moja na Mbili iwapo tunaweza kutumia maeneo mawili ya mpakati kati ya Uturuki na Syria. Na zaidi ya hapo tunaendelea kushuhudia shule na hospitali zikitumika kijeshi, kwa hiyo hakuna jambo moja tu la kuwa mwarubaini wa jambo hili.”

Bi. Amos amesema azimio namba 2139 la Baraza la Usalama lina mambo yote muhimu yanayopaswa kurahisisha kazi yao lakini tatizo ni utekelezaji.

Azimio hilo la mwaka jana linataka pande zote kwenye mzozo kuwezesha misaada ya kibinadamu kufikia walengwa na kuhakikisha raia hawanyimwi haki yao ya msingi ya kupata vyakula na dawa.