Umoja wa Mataifa waingia na wasiwasi kuhusu vurugu za Libya
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini kwa ajili ya kuipiga jeki Libya
imesema kuwa inaendelea kufuatilia kwa karibu yale yanayoendelea
kujitokeza katika taifa hilo hasa katika eneo la Benghazi. Taarifa zaidi na George Njogopa.
Katika taarifa yake UNSIMIL imelaani vikali mauwaji yanayoendelea
kwenye eneo hilo na kutoa wito kwa pande zinazozozana kujiepusha na
vurugu.
Kumekuwa na mlolongo wa mapigano baina ya makundi yanayohasimiana na
kusabisha watu kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa.
Hali ya waiswasi imeendelea kulikumba eneo hili na hakuna dalili ya
kupatikana suluhi kutokana na kuongezeka kwa matukio yanayoambatana na ugaidi
Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umezitaka mamlaka za kidola
kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo korofi ambayo inazidisha
kitisho kwa maisha ya raia.