Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka China iwaachie huru wanaharakati: Pillay

UN Photo - Jean-Marc Ferre
Bi. Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu. (

Pillay aitaka China iwaachie huru wanaharakati: Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelewa kuwepo kizuizini kwa watetezi wa haki za raia, wanasheria na waandishi wa habari nchini China.

Pillay ametoa wito huu wakati wa kuelekea kwenye kumbukumbu ya miaka 25 ya tukio la mwezi Juni 1989 kwenye bustani ya Tiananmen huko China akisisitiza pia umuhimu wa kuchunguza mazingira ya tukio hilo.

Nasihi mamlaka za China kuwaachia huru mara moja wale wanaoshikiliwa ili waweze kuwa na haki yao ya msingi ya kujieleza amesema Pillay.

Inadaiwa kuwa makumi kadhaa ya watu wanashikiliwa na mamlaka za China kabla ya kufanyika kwa kumbukumbu hiyo tarehe Jumatano tarehe Nne Juni kwa madai ya kusababisha ghasia waliposhiriki kwenye mjadala wa faragha kuhusu matukio ya Tiananmen.

Pillay amesema badala ya kuweka udhibiti bali China inapaswa kuchochea mashauriano na majadiliano kama njia ya kuondokana na mambo yaliyopita.

Mkuu huyo wa haki za binadamu amesema mengi ya tarehe 3 na 4 June mwaka 1989 hayafahamiki mathalani idadi kamili ya waliokufa na familia nyingi zinasubiri ukweli kuhusu kilichowapata wapendwa wao.

Amesema China imepata mafanikio makubwa ya kichumi na kijamii katika miaka 25 na kujifunza kutokana na matukio ya zamani hakutatokomeza mafanikio bali kutaonyesha vile nchi hiyo inalinda na kuheshimu haki za binadamu.