Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuundwa serikali mpya Palestina

Ban akaribisha kuundwa serikali mpya Palestina

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha tangazo la Rais Mahmoud Abbas la kuundwa kwa serikali mpya Palestina, ikiongozwa na Waziri Mkuu Rami Hamdallah.

Katika taarifa ilosomwa na msemaji wake kwa waandishi wa habari, Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukisisitiza haja ya kupiga hatua za kufikia umoja wa Palestina, kwa mujibu wa maazimio yaliyopo, na kutambua ahadi za Rais Abbas kuwa serikali yake itaendelea kuzingatia ahadi za kuitambua Israel, kujiepusha na ghasia, na kutimiza makubaliano kadha wa kadha. Stephane Dujarric ni msemaji wa Katibu Mkuu

“Umoja wa Mataifa u tayari kuunga mkono serikali mpya iliyoundwa katika juhudi zake za kuunganisha Ukingo wa Magharibi na Gaza, kulingana na makubaliano ya muungano wa Wapalestina wa Aprili 23, chini ya mamlaka halali za Palestina, pamoja na kushughulikia changamoto sugu za kisiasa, kiusalama, kibinadamu na kiuchumi za Gaza, na kufanya uchaguzi ambao umechelewa kwa muda mrefu. Mratibu maalum Roberty Serry aliyajadili masuala hayo na Waziri Mkuu, Hamdallah katika mkutano wao leo.”

Katibu Mkuu pia amesema kuwa chama cha PLO kitaendelea kuwa na wajibu wa kufanya mazungumzo ya amani na Israel, jambo ambalo limeridhiwa na Rais Abbas, huku akielezea matarajio yake kuwa fursa mpya za kupiga hatua za kufikia suluhu la mataifa mawili zitajitokeza hivi karibuni.