Wauguzi-wakunga na uokoaji wa maisha ya mama na mtoto wakimbizi huko Jordan:

Uhai wa mama na mtoto kwenye kambi ya wakimbizi ya Za'atari huko Jordan ni muhimu. (Picha@Unifeed)

Wauguzi-wakunga na uokoaji wa maisha ya mama na mtoto wakimbizi huko Jordan:

Migogoro inapotokea huduma za kijamii hususan za afya ya mama na mtoto zinakuwa mashakani na hivyo kusababisha ongezeko la vifo vya wajawazito na hata watoto. Shirika la Idadi ya watu duniani, UNFPA linasema kuwa pindi mizozo hiyo inapotokea inakuwa vigumu kupata madaktari lakini wakunga wanapokuwepo maeneo hayo wanakuwa sawa na watume waliotumwa na Mungu kwani wanasaidia kuziba pengo lililojitokeza. Miongoni mwao ni Munira Shaban anayehudumu katika kambi ya wakimbizi wa Syria ya Za’atari huko Jordan. Je anafanya nini? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.