Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wataka kushiriki katika kubuni mustakhbali wautakao

@Wambui Kahara

Vijana wataka kushiriki katika kubuni mustakhbali wautakao

Hapa mjini New York, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kongamano la vijana kuhusu kushirikishwa kwao kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 limeingia siku yake ya pili.

Vijana hao kutoka pembe zote za dunia wamekuwa wakijadiliana kuhusu masuala kadhaa yanayowahusu, yakiwemo uhaba wa ajira kwa vijana, na kuhusu jinsi ya kubuni mustakhbali wautakao, hususan ushiriki wao katika utungaji wa sera.

Mmoja wa washiriki kwenye kongamanohiloni Wamboi Kahara, mwakilishi wa vijana waKenyakwenye Umoja wa Mataifa, na amenieleza kile wanachosema viongozi na washiriki kwenye kongamanohilo

(Sauti ya Wambui)

Hapo jana, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon alisema kwamba vijana sio tena viongozi wa kesho, ila viongozi wa sasa. Nimemuuliza Wamboi ikiwa wanahisi kwamba wanashirikishwa ipasavyo katika uongozi.

(Sauti ya Wambui)