Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi maalum wa Ban kukutana na Waziri Mkuu mpya wa Palestina

UN Photos
Robert Serry @

Mwakilishi maalum wa Ban kukutana na Waziri Mkuu mpya wa Palestina

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mjakato wa amani Mashariki ya Kati, Robert Serry anatarajia kuwa na mkutano na Waziri Mkuu mpya  wa Palestina Rami Hamdallah hapo kesho.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric ameeleza kuwa mkutano huo unalenga kutafuta suluhu ya kudumu ya amani kwenye Ukanda wa Gaza na Ukingo wa mgharibi wa mto Jordan ili hatimaye kuwa na suluhu ya kuwa na mataifa mawili; Israeli na Palestina.

Amesema Umoja wa mataifa unaendelea kuangazia umoja wa Palestina kwa minajili ya ahadi yake ya kutambuaIsrael, na kutupilia mbali mashambulizi na kuheshimu makubaliano na hii ikiwa ni njia mojawapo  ya maendeleo ya ushirikiano.

Ameongeza kuwa maafikiano ya leo ya kuunda serikali ya muda  ya mapatano, ni kielelezo kinachoashiria lengo la upatanishi  wa ndani ya Palestina kwa maafikiano ya tarehe 23 mwezi Aprili.