Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar iendelee kujenga demokrasia, asema Mtaalam Maalum wa Umoja Wa Maifa.

UN Photos/Kibae Park
Wanafunzi Myanmar, @

Myanmar iendelee kujenga demokrasia, asema Mtaalam Maalum wa Umoja Wa Maifa.

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar bwana Tomas Ojea Quintana, ameihimiza serikali ya Myanmar kendelea na kuhakikisha kwamba msingi wa demokrasia uliowekwa miaka mitatu iliyopita umeimarika. Taarifa kamili na John Ronoh

TAARIFA YA JOHN

Bwana Quintana amesema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati alipokuwa akitamatisha kazi yake ya miaka sita nchini Myanmar, na kumkaribisha Mwakilishi mpya, Bi. Yanghee Lee,  kutoka Korea Kusini, ambaye anaichukuwa nafasi yake ya Mtaalam Maalum wa Umoja wa maitaifa wa haki za binadamu nchini humo.

Kwa miaka sita ya uhudumu wake, Myanmar  imenufaika na kuweka hitoria  kwa mabadiliko makuu ya uhuru , utangamano, na amani nchini.